TOKA NJE YA BOKSI

TOKA KWENYE NJE YA BOKSI Hapo zamani za kale alikuwepo kijana aliyepata ulemavu wa mguu,madaktari wakatoa ushauri kwa mzazi wake kuwa anatakiwa awekwe kwenye boksi kwa muda mrefu hadi atakapo pata nafuu. Mara kwa mara mzazi wake alikuwa anakwenda naye kila mahali atakapo kwenda. Baada ya muda mrefu, yule kijana alianzisha tabia ambayo hakumpendezea mzazi wake, kijana aligongagonga boksi ili aweze kutoka, siku moja aliweza kuligonga hadi likaanguka na akaweza kutoka nakutembea pekee yake. Alijifunza kutembea na akaweza kutembea vizuri kabisa. Huyu kijana alifanya kitu ambacho wengine walishangaa ambacho watu wengi hawakuamini kama inawezekana. Huyu kijana alikataa kukaa kwenye boksi ambalo mtu mwingine alimuweka ndani yake na akaamua atokee pekee yake. Kuna mtu au kitu kimekuweka kwenye boksi ambalo unataka kutoka. Toka sasa. Kila mmoja wetu anakutana na changamoto katka maisha. Jiandae kifikra kuzishinda hizo changamoto. Decide to rock your box until it falls apart. Baraka Damian Public and Motivational Speaker

Comments

Popular posts from this blog

MTAZAMO CHANYA vs MTAZAMO HASI

TAMBUA NGUVU ILIYOPO KATIKA FIKRA NA MANENO YAKO

Kwa nini tunafanya kazi