CHAGUA KUWA NA FURAHA

CHAGUA KUWA NA FURAHA
Furaha ni changuo.
Ndugu mpendwa na msomaji ya makala haya.
Leo tutaongelea kuwa na furaha maishani.
Maisha yetu yanahitaji tuwe na furaha kila mara lakini ni vigumu kuwa na furaha wakati wote.
Furaha ndio inasababisha tufanye kazi vizuri. Huzuni ni adui mkubwa wa mafanikio.
Tunapitia mambo makubwa na magumu katika maisha yetu lakini kuhuzuni hakuwezi kubadili changamoto hizo tunazokutana nazo kila siku.
Kwa hiyo badala ya kuhuzunika tunatakiwa tuchague kuwa na furaha hata kwenye magumu yote tunayopitia kila siku.
Furaha ni uamuzi unaoamua kufanya na wala siyo hisia unazokuwa nazo.
Kuna vitu maishani mwetu hatuwezi kuvibadilisha kwa hiyo tunatakiwa tukubaliane navyo ili maisha yaendelee.
Maisha ni zawadi tuliyopewa na Mungu ni lazima tufurahi hiyo zawadi tuliyopewa.
Baraka Damian
Public and Motivational Speaker
+255712360145
Sambaza kwa watu wengine pia.

Comments

Popular posts from this blog

MTAZAMO CHANYA vs MTAZAMO HASI

TAMBUA NGUVU ILIYOPO KATIKA FIKRA NA MANENO YAKO

Kwa nini tunafanya kazi