" Ili ufanikiwe, nia ya kufanikiwa inatakiwa kuwa kubwa kuliko uwonga wa kushindwa"
Baraka Damian Machumu
Email me:machumubaharack@gmail.com
+255712360145
Tarehe 21/01/2017 Mambo niliyojifunza kutoka kitabu cha "Why we work kilichoandikwa na Barry Schwartz Kila mtu ana sababu kwa nini anafanya kazi 1. Tunafanya kazi ili tuwe na furaha katika maisha yetu. Mtu ambaye anafanya kazi ana furaha. 2. Kazi ni kipimo cha ushirikiano. Ili uonekane kuwa una ushirikiano na watu au jamii yako lazima ufanye kazi. 3. Mabadiliko katika sehemu za kazi. Mabadiliko katika sehemu za kazi hatuyapati kwa siku moja yanahitaji muda lakini tunatakiwa tuendelee kufanya kazi tusisumbilie yawe vizuri. 4. Uzoefu. Katika maisha yetu kufanya kazi umekuwa ni uzoefu wa muda mrefu tunafanya kazi kwa ajili ya kupata pesa wakati wengine wanafaidika na kazi tunazofanya.. 5. Kufungamana na kazi unayoifanya. Ili kuwe na matokeo chanya lazima ufungamane na kazi unayoifanya. 6. Dhamira(meaningful) kwenye kazi. Kuwa dhamira au kusudi nzuri katika kazi unayoifanya hata kwenye magumu utasimama kutekeleza kazi yako. 7. Kuchukua majukumu. Kwa wale tunapata nafasi y...
Habari ndugu na rafiki, Kwanza, napenda kuwashukuru wote ambao umekuwa mkisoma makala yangu katika mwaka huu Pili, napenda kuwajulisha kuwa kati ya makala nitakazoziandika mwisho mwa mwaka itakuwepo makala ya vitabu nilivyosoma mwaka huu Niwatakie sherehe njema na baraka tele tunapomaliza mwaka huu. Mambo niliyojifunza kutoka katika kitabu LEAD THE FIELD kilichoandikwa na EARL .N. 1. Kila binadamu ameumba na uwezo mkubwa wa kutengeneza maisha yake mwenyewe. Hakuna mtu ambaye atafanikiwa kisa ndugu yake au baba au mama yake amefanikiwa. 2. Kufanikiwa au kushindwa kwa binadamu hahitaji bahati au mazingira. Kufanikiwa ni lazima kuachana na mitazamo hasi tuliyonayo katika jamii yetu. 3. Mtazamo wako. Mtazamo wako ni mchango mkubwa sana katika mafanikio yako ya kila siku. Unatazamaje changamoto unazokutana nazo kila siku kwenye biashara yako. Changamoto zipi unakutana nazo na namna gani unakabiliana nazo kwa namna ipi? 4. Kanuni na taratibu. Ili uweze kufanikiwa lazima uweze kufuata tarat...
MTAZAMO CHANYA Mpendwa rafiki Kila mtu anakutana na changamoto mbalimbali katika maisha ya kila siku.Uwe ni mfanyakazi umeajiriwa na kampuni kubwa au mfanyabiashara au hauna kazi kukutana changamoto ni jambo la kawaida. Kuna changamoto za aina mbalimbali unazokutana nazo ambazo zinakufanya urudi nyuma katika malengo yako. Changamoto uliyonayo si kitu pale tu utaweza kujenga fikra chanya au mtazamo chanya kwenye kila changamoto unayokutana nayo. Fundisha akili yako kuwa na uwezo mkubwa wa kukabiliana na misukosuko ya maisha. Ili uweze kufanikiwa kwenye jambo lolote unalolifanya jenga mtazamo chanya kwenye kufanikiwa hilo jambo hilo. Kumbuka hakuna mtu hata mmoja atakayekuja kusaidia kwenye matatizo yako.Acha kulalamika hayo ni maisha yako,fanya maamuzi juu ya maisha yako. Tukutane tena kesho. Baraka Damian Public and Motivational Speaker 0712360145
Comments
Post a Comment