TABIA YAKO NDIO MAFANIKIO YAKO
TABIA YAKO NDIO MAFANIKIO YAKO
Ndugu na rafiki mpendwa
Karibu sana katika makala ya leo
Makala ya leo inazungumzia kuhusu tabia tulizonazo namna gani zinachangia katika mafanikio yetu kwa ujumla.
0653783164
Nakuomba uendelea kusoma makala katika blogu ili uweze kunufaika zaidi.
Ndugu na rafiki mpendwa
Karibu sana katika makala ya leo
Makala ya leo inazungumzia kuhusu tabia tulizonazo namna gani zinachangia katika mafanikio yetu kwa ujumla.
Moja kati ya kazi za lazima ambazo hutakiwi kukosa kuzifanya kwenye kila siku ambayo Mungu amekupa. Ni kazi zinazokujengea tabia mpya(tabia chanya). Tofauti kati yako wewe na malengo yako iko tabia zako,haiwezekani ukatimiza malengo yako uliyonayo ukiwa tabia hizo ulizonazo sasa(tabia hasi).
Moja kati ya mchakato muhimu unaohitaji kuupitia kwa sasa ili uweze kutimiza malengo yako uliyonayo,unahitaji kujenga tabia mpya zinzzoendana na malengo uliyonayo. Na ili uweze kujenga tabia mpya utahitaji ubadilishe ratiba yako ya kila siku,yaani ni kwamba kuna mambo yale unayoyafanya mara kwa mara na tena kila siku kwa sababu ya tabia yako yanakuwa ni matendo yako ya kila siku.
Moja kati ya kitu unachotakiwa kufanya kubadilisha hali hiyo,kazi mpyalazima uifanyee ndani ya siku yako na utakiwa uifanye makusudi kabisa ili kuua tabia ya zamani kwa maana tabia hii ni mpya lazima uifanye kwa nguvu zako zote. Kufanya mara kwa mara na kuendelea kufanya inakuwa ni tabia yako. Muonekano wako pia hubadilika na maisha yako pia hubadilika na malengo yako hutekelezeka.
Kwahiyo pamoja na ufinyu wa muda hakikisha ulionao unazitambua kazi mpya kutokana na malengo yako uliyonayo nahakikisha unazifanyia kazi kila inapoitwa leo.
Imeandikwa na:
Charles Kwiyukwa0653783164
Nakuomba uendelea kusoma makala katika blogu ili uweze kunufaika zaidi.
Comments
Post a Comment