Kwa nini tunafanya kazi

Tarehe 21/01/2017 Mambo niliyojifunza kutoka kitabu cha "Why we work kilichoandikwa na Barry Schwartz Kila mtu ana sababu kwa nini anafanya kazi 1. Tunafanya kazi ili tuwe na furaha katika maisha yetu. Mtu ambaye anafanya kazi ana furaha. 2. Kazi ni kipimo cha ushirikiano. Ili uonekane kuwa una ushirikiano na watu au jamii yako lazima ufanye kazi. 3. Mabadiliko katika sehemu za kazi. Mabadiliko katika sehemu za kazi hatuyapati kwa siku moja yanahitaji muda lakini tunatakiwa tuendelee kufanya kazi tusisumbilie yawe vizuri. 4. Uzoefu. Katika maisha yetu kufanya kazi umekuwa ni uzoefu wa muda mrefu tunafanya kazi kwa ajili ya kupata pesa wakati wengine wanafaidika na kazi tunazofanya.. 5. Kufungamana na kazi unayoifanya. Ili kuwe na matokeo chanya lazima ufungamane na kazi unayoifanya. 6. Dhamira(meaningful) kwenye kazi. Kuwa dhamira au kusudi nzuri katika kazi unayoifanya hata kwenye magumu utasimama kutekeleza kazi yako. 7. Kuchukua majukumu. Kwa wale tunapata nafasi ya kutengeneza kazi kwa watu wengine tutengeneze mazingira mazuri kwa wao kufanya kazi. 8. Thamani ya kila mmoja katika kazi. Lazima tutengeneze mazingira ya kila mmoja kuona thamani ya kazi yake kwenye eneo lake. 9. Msukumo. Kuna msukumo uliko ndani yetu unatusukuma kufanya kazi fulani japo pia kuna msukumo wa nje pia. 10. Malipo. Watu wengi kwa sasa wanafanya kazi fulani kwa sababu kuna malipo kutoka kwenye hiyo kazi.

Comments

Popular posts from this blog

MTAZAMO CHANYA vs MTAZAMO HASI

TAMBUA NGUVU ILIYOPO KATIKA FIKRA NA MANENO YAKO