BADILI CHANELI(CHANGE THE CHANNEL)

BADILI CHANELI(CHANGE THE CHANNEL)
Wote tunajua kutumia rimoti (remote controler) kubadili chaneli kwenye TV zetu. Kama ukiangalia kitu ambacho hukipendi hakuna shida unabadili chaneli na kuweka chaneli nyingine ambayo utapata kitu unachokipenda kukitazama kwa wakati huo.
Tunatakiwa tujifunze namna ya kubadili chaneli za fikra zetu pale tunapokutana na mtazamo wa fikra hasi kwenye maisha yetu ya kila siku.
Kwq hali ya kushangaza hii hali ikitokea kwa watu wengi hulizika nayo badala kubadilisha chaneli zao za mtazamo kutoka mtazamo hasi kwenda mtazamo chanya wao huvuta viti na kukaa na kuangiza vinywaji wanavyovipendelea na kuendelea kuburudika wakiendelea kutazama chaneli ileile ambayo huipendi. Unakumbuka maumivu na mateso uliyopitia zamani. Unapoteza furaha na amani moyoni mwako.
Jifunze kubadili chaneli ya fikra  ambayo huipendi, ambayo inakuletea mawazo hasi, mawazo yanayokubomoa na kukupotezea nguvu zako zote.
#Tazama mambo mazuri ambayo umeshawahi fanya
#Tambua wewe ni wa tofauti hakuna kama wewe katika uso wa dunia hii.
#Jifunze kubadili changamoto zako kuwa fursa katika maisha yako.
Let change your mindset.
Baraka Damian
Public and Motivational Speaker
0712360145

Comments

Popular posts from this blog

MTAZAMO CHANYA vs MTAZAMO HASI

TAMBUA NGUVU ILIYOPO KATIKA FIKRA NA MANENO YAKO

Kwa nini tunafanya kazi