Uchambuzi wa kitabu cha Lead the field
Habari ndugu na rafiki,
Kwanza, napenda kuwashukuru wote ambao umekuwa mkisoma makala yangu katika mwaka huu
Pili, napenda kuwajulisha kuwa kati ya makala nitakazoziandika mwisho mwa mwaka itakuwepo makala ya vitabu nilivyosoma mwaka huu
Niwatakie sherehe njema na baraka tele tunapomaliza mwaka huu.
Mambo niliyojifunza kutoka katika kitabu LEAD THE FIELD kilichoandikwa na EARL .N.
1. Kila binadamu ameumba na uwezo mkubwa wa kutengeneza maisha yake mwenyewe. Hakuna mtu ambaye atafanikiwa kisa ndugu yake au baba au mama yake amefanikiwa.
2. Kufanikiwa au kushindwa kwa binadamu hahitaji bahati au mazingira. Kufanikiwa ni lazima kuachana na mitazamo hasi tuliyonayo katika jamii yetu.
3. Mtazamo wako. Mtazamo wako ni mchango mkubwa sana katika mafanikio yako ya kila siku. Unatazamaje changamoto unazokutana nazo kila siku kwenye biashara yako. Changamoto zipi unakutana nazo na namna gani unakabiliana nazo kwa namna ipi?
4. Kanuni na taratibu. Ili uweze kufanikiwa lazima uweze kufuata taratibu na sheria kwenye kila unachokifanya.
5. Mazingira. Mazingira uliyopo ndio yatakayo kufanya ufanikiwe. Mazingira ni kama kioo kile unachoweka ndo unachopata. Ukiweka kitu kizuri kinatoa kizuri,ukiweka kibaya utapata kitu kibaya.
6. Tabia. Tabia uliyonayo ndio tabia ya watu wanaokuzunguka nao wako hivyo hivyo. Ukibadili tabia watu wanaokuzunguka nao hubadilika.
7. Maliasili watu. Ili uweze kufanikiwa inatakiwa uwekeze kwa watu. Na kitu unachokifanya lazima ukifanye kupitia watu.
8. Uhuru. Sehemu ambayo watu wana uhuru wa kufanya jambo lolote kwa uhuru,mafanikio nayo yapo pia.
9. Juhudi. Kwenye kila jambo kama kuna juhudi lazima utafanikiwa.
10. Maono. Lazima uwe na maono na kitu unachokifanya kwenye kila jambo. Maono yanakuongoza kupeleka kwenye mafanikio.
11. Mipango. Weka mipango kufikia malengo unayoyataka katika maisha yako.
12. Kuwa na malengo yanayofikika. Panga na weka malengo ambayo utayafikia kulingana na muda husika.
13. Tatua matatizo. Tambua na tatua matatizo yako wewe mwenyewe,hakuna atakayekuja kutatua matatizo yako.
14. Ushauri. Ili uweze kufanikiwa lazima utafute mtu wa kushauri ili uweze kufanikiwa na kufikia malengo.
15. Fundisha akili yako. Tenga muda wa kufundisha akili yako kwenye malengo na maono yako.
16. Mafanikio yanachukua muda. Hakuna mafanikio yanayotokea kwa siku moja tu. Inachukua muda kufanikiwa kwenye kila jambo.
17. Lipa bei. Lipa gharama ya kupata mafanikio unayoyapata katika biashara yako.
Imeandikwa na
Rafiki yako
BDamian
Public and motivational speaker
+255 712 360 145
Fb: Baharack Machumu
http://machumumaere.blogspot.com
Comments
Post a Comment