TUMAINI KWENYE MAISHA

TUMAINI KWENYE MAISHA.

Ndugu na rafiki yangu mpendwa,
Leo katika makala yangu nitaongelea umuhimu wa kuwa na tumaini kwenye maisha.
Tumaini ni hali ya akili kutarajia mambo chanya yatatokea ukihusisha na hali ya maisha ulionayo kwa sasa.
Ninajua kwa sasa unapitia mambo hali gumu na changamoto kwenye maisha yako. Umefujikafujika na changamoto za kila siku.
Kitu ninachoweza kukuambia kuwa ni vyema uwe na tumaini kwenye maisha yako kuwa ipo siku mambo yatakuwa na wewe utafanikiwa kwenye maisha.Kuwa na tumaini kuwa hayo matatizo na changamoto unazopitia kwa sasa ipo siku yataisha.
Utakapo kuwa na tumaini kwenye maisha yako itakusaidia kuendelea kupambana na changamoto za kila siku na utakuwa mshindi.
  • Kesho na tumaini.Kesho na tumaini vinaenda pamoja bila tumaini hakuna kesho katika maisha yako.
  • Tumaini inahamasisha. Ukiwa na tumaini utahamasika kufanya kazi kwa bidii.
Tumaini inakupatia nguvu ya kukanyanga kesho kwa kishindo. Nakuomba uwe na tumaini kwenye maisha yako.

Baraka DM
Public and Motivational Speaker
+255712360145

Comments

Popular posts from this blog

MTAZAMO CHANYA vs MTAZAMO HASI

TAMBUA NGUVU ILIYOPO KATIKA FIKRA NA MANENO YAKO

Kwa nini tunafanya kazi