TEMBEA NA WATU SAHIHI
TEMBEA NA WATU SAHIHI
Ndugu na rafiki yangu
Leo ni siku nyingine tena ambayo mwenyezi Mungu ametupatia ili tufanye jambo ambalo ametuitia kwenye uso huu wa dunia.
Ili tuweze timiza ndoto zetu kuna jambo moja nahitaji tujadili ili kutufanikisha kutimiza malengo na ndoto zetu.
Mahusiano ni jambo ambalo ni muhimu sana katika maisha ya mwanadamu. Kila siku unahusiana na watu mbalimbali ili tuweze kufanikisha malengo na jambo lolote lilopo mbele yetu. Lakini siyo kila mahusiano ni mazuri.
Lazima tuangalie ni watu gani tunahusiana nao,wengine hawawezi kusaidia kufikia malengo yako.
Tunatakiwa tuhusiane na watu ambao wamefanikiwa na pia wanahamasa ya kufanya kazi kwa bidii. Watu ambao wana mawazo hasi watazima mto ulioko kwenye fikra zako. Kama kweli umeanza safari hii ya mafanikio lazima utafute watu watakusaidia kufikia kule unakotaka kwenda bila kuchelewa. Hata kama ni familia yako lakini hakuhamasishi kufikia ndoto zako acha nao ila waheshimu maana ndio ndugu zako pekee. Watu tunaohusiana nao wana uwezo mkubwa sana kutufanya tufanikiwe. Ukweli ni kwamba ndugu na rafiki wana mchango mkubwa katika maisha yetu na pia kwenye mafanikio yetu. Lazima tufanyie kazi kuwa watu wazuri wa kuhusiana nao.
Nikutakie siku njema na yenye mafanikio tele. Pia mafanikio makubwa kwa kile ulichoanza kufanya sasa.
Baraka DM
Public and Motivational Speaker
Watsupp me:+255 712360145
Comments
Post a Comment