NGUVU YA MUDA
Ndugu wasomaji makala zangu. Leo napenda kuwashirikisha makala nzuri ya NGUVU YA MUDA. Makala hizi zitakuwa za mfululizo zikizungumzia mafanikio katika kutumia muda kwa hekima na busara.
Karibuni kwa siku ya leo.
Kila binadamu anayeishi katika dunia hii ana muda sawa na mwenzake awe ni fukara au tajiri wote wana muda sawa. Ila kitu kinacho tutofautisha ni namna tunavyoutumia muda. Kama wote tungeweza kutumia kwa hekima na busara kubwa tungefanikiwa kufanikiwa katika nyanja ya kutumia muda vizuri.
Muda ni rasimali ambayo inakwisha na hairudi tena. Tumekuwa tukifanya kazi ila muda hutoshi ni kwa sababu hatujajua namna ya kutumia muda kwa busara.
Katika makala hizi tunaendelea kujifunza mbinu za kutumia muda vizuri. Niwatie moyo tu kuwa kutumia muda vizuri ni ujuzi unajifunzwa. Karibuni kwa kujifunza katika mada hii ya NGUVU YA MUDA.
Ni Mimi rafiki yako
Mwandishi
Baraka D Machumu.
Comments
Post a Comment