MTAZAMO CHANYA vs MTAZAMO HASI. Kiwanda kikubwa cha uzalishaji wa viatu kiliwatuwa watu wawili kufanya utafiti wa soko la viatu kwenye sehemu moja. Majibu yao ya utafiti yalikuwa kama hivi: Mtu wa kwanza: Huku hakuna soko la viatu maana hakuna mtu anayevaa viatu. Mtu wa pili: Huku kuna soko kubwa la viatu maana hakuna mtu hata mmoja aliyevaa viatu. Mtazamo hasi unaficha fursa iliyopo kwenye mazingira yako. Mtazamo chanya unakuonesha fursa kubwa iliyopo kwenye mazingira yako. Fundisha akili yako kuwa na mtazamo chanya. Baraka Damian +255 712 360 145 http://machumumaere.blogspot.com
TAMBUA NGUVU ILIYOPO KATIKA FIKRA NA MANENO YAKO. Ndugu,rafiki na msomaji wa makala zangu Leo ni siku nyingine tena ambayo nakuletea makala hii nzuri ya jinsi gani ya kutambua nguvu iliyopo katika fikra na maneno unayojisemea wewe mara kwa mara. Kama unahitaji kuishi maisha yenye furaha na amani lazima utambue nguvu iliyoko ndani yako. Nguvu ambayo unaitoa kila siku juu yako wewe mwenyewe. Fikra unazofikiria kila mara ndio matokeo halisi yanayotokea katika maisha yako. Kama ukiendelea kushikiria mawazo hasi,utaendelea pata matokeo hasi kwenye kila nyanja unayojaribu kufanya, utazungukwa na watu wenye mawazo au fikra hasi. Hutaweza kufanikisha malengo yako. Maisha hufuata fikra zako. Kama unafikiria mawazo chanya,mawazo ya kufanikiwa,yenye furaha utakuwa mtu mwenye furaha na utaweza kuchukuliana na changamoto zote zinazotokea katika maisha yako. Tambua kuwa hakuna mtu yeyote ambaye anaweza kukupangia kitu cha kufikiria ila wewe mwenyewe ndiye mtawala wa fikra na mawazo yako yote.
Tarehe 21/01/2017 Mambo niliyojifunza kutoka kitabu cha "Why we work kilichoandikwa na Barry Schwartz Kila mtu ana sababu kwa nini anafanya kazi 1. Tunafanya kazi ili tuwe na furaha katika maisha yetu. Mtu ambaye anafanya kazi ana furaha. 2. Kazi ni kipimo cha ushirikiano. Ili uonekane kuwa una ushirikiano na watu au jamii yako lazima ufanye kazi. 3. Mabadiliko katika sehemu za kazi. Mabadiliko katika sehemu za kazi hatuyapati kwa siku moja yanahitaji muda lakini tunatakiwa tuendelee kufanya kazi tusisumbilie yawe vizuri. 4. Uzoefu. Katika maisha yetu kufanya kazi umekuwa ni uzoefu wa muda mrefu tunafanya kazi kwa ajili ya kupata pesa wakati wengine wanafaidika na kazi tunazofanya.. 5. Kufungamana na kazi unayoifanya. Ili kuwe na matokeo chanya lazima ufungamane na kazi unayoifanya. 6. Dhamira(meaningful) kwenye kazi. Kuwa dhamira au kusudi nzuri katika kazi unayoifanya hata kwenye magumu utasimama kutekeleza kazi yako. 7. Kuchukua majukumu. Kwa wale tunapata nafasi y
Comments
Post a Comment