TAMBUA NGUVU ILIYOPO KATIKA FIKRA NA MANENO YAKO. Ndugu,rafiki na msomaji wa makala zangu Leo ni siku nyingine tena ambayo nakuletea makala hii nzuri ya jinsi gani ya kutambua nguvu iliyopo katika fikra na maneno unayojisemea wewe mara kwa mara. Kama unahitaji kuishi maisha yenye furaha na amani lazima utambue nguvu iliyoko ndani yako. Nguvu ambayo unaitoa kila siku juu yako wewe mwenyewe. Fikra unazofikiria kila mara ndio matokeo halisi yanayotokea katika maisha yako. Kama ukiendelea kushikiria mawazo hasi,utaendelea pata matokeo hasi kwenye kila nyanja unayojaribu kufanya, utazungukwa na watu wenye mawazo au fikra hasi. Hutaweza kufanikisha malengo yako. Maisha hufuata fikra zako. Kama unafikiria mawazo chanya,mawazo ya kufanikiwa,yenye furaha utakuwa mtu mwenye furaha na utaweza kuchukuliana na changamoto zote zinazotokea katika maisha yako. Tambua kuwa hakuna mtu yeyote ambaye anaweza kukupangia kitu cha kufikiria ila wewe mwenyewe ndiye mtawala wa fikra na mawazo yako yote. ...
Comments
Post a Comment