Habari ndugu na rafiki, Kwanza, napenda kuwashukuru wote ambao umekuwa mkisoma makala yangu katika mwaka huu Pili, napenda kuwajulisha kuwa kati ya makala nitakazoziandika mwisho mwa mwaka itakuwepo makala ya vitabu nilivyosoma mwaka huu Niwatakie sherehe njema na baraka tele tunapomaliza mwaka huu. Mambo niliyojifunza kutoka katika kitabu LEAD THE FIELD kilichoandikwa na EARL .N. 1. Kila binadamu ameumba na uwezo mkubwa wa kutengeneza maisha yake mwenyewe. Hakuna mtu ambaye atafanikiwa kisa ndugu yake au baba au mama yake amefanikiwa. 2. Kufanikiwa au kushindwa kwa binadamu hahitaji bahati au mazingira. Kufanikiwa ni lazima kuachana na mitazamo hasi tuliyonayo katika jamii yetu. 3. Mtazamo wako. Mtazamo wako ni mchango mkubwa sana katika mafanikio yako ya kila siku. Unatazamaje changamoto unazokutana nazo kila siku kwenye biashara yako. Changamoto zipi unakutana nazo na namna gani unakabiliana nazo kwa namna ipi? 4. Kanuni na taratibu. Ili uweze kufanikiwa lazima uweze kufuata tarat...
Comments
Post a Comment